Arsenal walivyoanza kugombea nafasi ya makundi champions league dhidi ya Besiktas


Mechi za awali za michuano ya kombe la mabingwa wa ulaya za kugombea kuingia kwenye hatua za makundi ya michuano mikubwa zaidi kwa ngazi ya vilabu barani ulaya ilianza jana, huku mchezo wa Arsenal dhidi ya Besiktas ya Uturuki ukitawala kwenye vichwa vya habari vya vyombo vya habari duniani kote.

Mchezo huo uliochezwa usiku wa jana uliisha kwa Arsenal kupata sare tasa ugenini kwenye dimba la Ataturk. 
Demba Ba aliwasumbua sana Arsenal na kwenye sekunde ya kwanza tu ya mchezo alimfanya kipa Szczesny kufanya kazi ya ziada kuokoa mchomo wake wa kutoka katikati ya uwanja, dakika kadhaa baadae Demba Ba aliunganisha krosi safi ya Ozyakup lakini umahiri wa Szczesny ukaiokoa tena Gunners.

Aaron Ramsey hakuweza kumaliza mechi baada ya kupewa kadi nyekundu na hivyo ataukosa mchezo wa marudiano jumatano ijayo. 


No comments